Askofu Malasusa: Huduma za kibenki zifikie makundi yaliyosahaulika

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa amesema mafanikio ya benki ni kujenga mazingira wezeshi ya kuwafikia wananchi waliosahaulika katika huduma za kifedha kwa kuwapa elimu sahihi ya kifedha na kunufaika na mikopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.