Skimu ya umwagiliaji kunufaisha wakulima 24,500 Mwanga

Wananchi wa Kata ya Kigonigoni, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa mradi wa skimu ya umwagiliaji unaoendelea katika eneo hilo, wakisema kukamilika kwake kutawasaidia kujikwamua kiuchumi na kupunguza umaskini.