Wafanyakazi kiwanda cha chai Kibena wagoma, kisa mshahara

Zaidi ya wafanyakazi 250 wa Kiwanda cha Chai cha Kibena Tea Ltd mkoani Njombe, wameanza mgomo wa kutokwenda kazini wakishinikiza kulipwa malimbikizo ya mishahara pamoja na michango yao ya hifadhi ya jamii.