Soko la Kasera lakumbwa na anguko la bei ya Samaki, mfungo watajwa sababu
Wavuvi na wachuuzi wa Soko Kuu la Kasera jijini Tanga wamelalamikia kushuka kwa bei ya samaki na kupungua kwa idadi ya wateja, wakihusisha hali hiyo na kuingiliana kwa vipindi vya mfungo wa Kwaresma na Ramadhani.