Ulega: Babarara Mlima Kitonga kuwa njia nne

Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza upanuzi wa barabara ya Kitonga mkoani Iringa, ambayo sasa itakuwa ya njia nne na yenye taa za barabarani. Mkakati huo unatajwa kuwa licha ya kuboresha huduma, lakini pia unakwenda kumaliza ajali kwenye eneo hilo.