MFUASI wa chama cha DP amejeruhiwa baada ya vurugu kuzuka katika uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani cha Evurore. Kelvin Mwenda, ambaye ndiye ajenti mkuu wa mwaniaji wa DP Albert Kigoro alipata majeraha kichwani wakati wahuni walipomvamia akiwa katika kituo cha kupiga kura cha Njarage Primary. Hofu ilitanda katika eneo hilo wakati ghasia zilipo zuka katika kituo hicho cha kura. Mwenda anadaiwa kupigwa huku akiendelea na shughuli zake katika kituo hicho. Anasemekana kuwa akifanya kazi yake ya uangalizi wakati wahuni hao walipomvamia na kumpiga. “Nilikuwa nafanya majukumu yangu ya uangalizi kama ajenti mkuu wa mwaniaji wa DP Albert Kigoro wakati kundi la wahuni liliponijia na kunipiga,” akahadithia.