Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imetakiwa kuwaandaa Watanzania kushiriki kikamilifu katika miradi ya mafuta na gesi, ikiwemo mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG), kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayowapa fursa ya kunufaika na utekelezaji wa miradi hiyo. Agizo hilo limetolewa mkoani Morogoro na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, katika …