Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limefafanua madai yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kupotea kwa watuhumiwa wanne wanaodaiwa kushikiliwa na jeshi hilo, likisisitiza kuwa, hakuna aliyepotea mikononi mwa polisi, bali baadhi yao wanatafutwa kwa kuvunja masharti ya dhamana na tuhuma za mauaji.