Orengo asema Oburu hana sifa za kuongoza ODM

GAVANA wa Siaya, James Orengo, amemkosoa vikali kiongozi wa ODM Dkt Oburu Odinga akisema hana sifa za kuongoza chama hicho. Bw Orengo alidai kuwa Dkt Oburu amebadilisha ODM kuwa bidhaa ya biashara kwa maslahi yake ya kibinafsi Akiwa na historia ya kupigania demokrasia na kupambana na utawala wa chama kimoja, Orengo alikuwa nguzo muhimu katika siasa za aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga. Kama mshauri mkuu wa kisheria wa Odinga na miongoni mwa waliosaidia kuunda Serikali ya Muungano wa Kitaifa mwaka 2008, Orengo amekuwa katika ODM kwa miaka mingi. Lakini sasa, anaonekana kubadilika huku akimpiga vita Dkt Oburu Katika mahojiano ya kina na Taifa Jumapili, Orengo alisema Dkt Oburu, kaka mkubwa wa Raila na seneta wa kaunti yake, hafai kuongoza ODM. "Oburu hajawahi kuonja gesi ya kutoa machozi," Orengo alisema, akiongeza kuwa Dkt Oburu hajawahi kukamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi wala kudhulumiwa kwa kutetea demokrasia ambayo ni msingi wa ODM. Orengo alisema kuwa watu kama Oburu, ambao hawajawahi kuweka maisha yao kwenye hatari kama alivyofanya Raila, hawawezi kuongoza ODM kwa manufaa ya chama na nchi nzima. "Hatuwezi kuwa na viongozi wa 'kibiashara' ambao wanatafuta faida yao binafsi," alisema Orengo akiashiria hali inayozidi kuwa mbaya katika ODM kutokana na viongozi wanaohusishwa na maslahi ya kifedha na uongozi wa kifamilia. Hali hii imemfanya Orengo kujiunga na vuguvugu la "Linda Mwananchi" linaloongozwa na Edwin Sifuna, akisisitiza kuwa ODM inahitaji kiongozi wa kweli, si "viongozi wa mikataba" ya maslahi ya kifedha badala ya maslahi ya chama na umma. Orengo pia alikosoa makubaliano ya serikali jumuishi akisema kuwa sio muungano wa kweli wa kisiasa lakini ni mpango ambao baadhi ya watu wamejiunga na serikali ya Kenya Kwanza. Alipinga serikali jumuishi akisema kuwa ODM kama chama hakiko kwenye serikali, na kwamba serikali ya sasa haifai kujiita jumuishi kwa kuwa haijaundwa kama iliyokuwa ya muungano mkuu mwaka wa 2008, ambapo kulikuwa na usawa wa madaraka kati ya Rais na Waziri Mkuu. Alieleza kuwa, wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta, kulikuwa na tume ya usimamizi wa muungano inayoshughulikia usawa na ushirikiano wa vyama, lakini sasa, ODM inazidi kupoteza mwelekeo. "Sisi ni wapinzani kwa kila namna lakini hatupaswi kuwa waoga wala kujificha. ODM inahitaji kiongozi ambaye anajua kusimamia mambo kwa ufanisi," alisema Orengo. Orengo alionekana kutokuwa na wasiwasi kuhusu kupoteza kiti cha kisiasa bila Raila Odinga akisema kwamba kuna sehemu fulani za ODM ambayo haitaweza kushinda bila uwepo wa Odinga, lakini akaweka wazi kuwa kama ODM itajiimarisha na kutokubali kutumiwa na wafanyabiashara wa siasa, inaweza kuvuma siku zijazo. "ODM haipaswi kutumika kama chama cha kutafuta maslahi binafsi. Kama tutakuwa na viongozi wa kweli, tutarudi katika mwelekeo sawa" alisema Orengo. Akijibu swali kuhusu uwezekano wa kugombea urais, gavana huyo alisema kwamba hiyo, atahakikisha ODM ni chama chenye nguvu, na kwamba kama kutakuwa na nafasi ya kuongoza, atachukua jukumu hilo kwa kujitolea. "Wakati ukifika, nitakuwa tayari kuchukua hatamu za uongozi kwa sababu ninajua kwa nini ninapigana," alisema Orengo. Kuhusu uhusiano na familia ya Odinga, hasa Dkt Oburu Oginga na madai ya baadhi ya viongozi wa ODM kwamba anaona wivu kwa kukosa kiti cha Oburu chamani Bw Orengo alisema, "Sina wivu. Ninachojali ni kwamba ODM isiwe mikononi mwa wanasiasa wanaoshikilia tu nafasi kwa manufaa yao binafsi.” Orengo alisisitiza kuwa chama cha ODM hakiwezi kurudi nyuma au kupoteza maadili na akataka wafuasi kujiandaa kwa uongozi wa kweli ambao watajitolea kwa maslahi ya chama na taifa. Aliweka wazi kuwa kama ODM itapoteza maadili yake, itakuwa ni sawa na kifo cha kisiasa. "ODM inahitaji mabadiliko ya kifikra na imani mpya. Huu si wakati wa kuwa na viongozi wanaotafuta tu maslahi yao binafsi. Tunahitaji viongozi wa kweli," alisema Orengo. Kuhusu ushirikiano na upinzani, Orengo alikiri kuwa ODM lazima ifanye kazi na vyama vingine, lakini alionya kuwa isiwe ni maslahi ya kibiashara bali ya kipekee kwa maendeleo ya taifa. "ODM inapaswa kuwa chama cha watu wa kawaida na sio chama cha biashara. Tumepambana sana kupata mfumo wa vyama vingi, tusikubali