Ajali ya ambulensi yaua mgonjwa, wanne wakijeruhiwa Korogwe

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Zaharia Abraham (41), mkazi wa Goha wilayani Korogwe, mkoani Tanga, amefariki dunia kufuatia ajali ya gari la wagonjwa lililokuwa likimsafirisha kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya matibabu, kugongana uso kwa uso na gari la mizigo.