Dk Mwigulu aagiza vitendea kazi vya bodaboda na mama lishe visishikiliwe

Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, amezitaka halmashauri, majiji, manispaa na vyombo vyote vinavyohusika na udhibiti kuacha kuwanyanyasa wajasiriamali wadogo, wakiwemo waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe, na badala yake waachwe wafanye shughuli zao kwa uhuru.