Mzee Samagubi alivyonusurika kifo, kaya 720 zikizongwa na maji Turiani
Zaidi ya kaya 700 zimekumbwa na mafuriko baada ya mto Mbulumi kuvunja kingo zake na kuelekeza maji katika makazi ya watu, hali iliyosababisha nyumba zaidi ya 20 kubomoka na wananchi kulazimika kukimbia makazi yao kuokoa maisha.