Mzozo Mashariki ya Kati wapandisha bei ya mafuta

BEI ya mafuta imepanda leo Jumatatu huku masoko ya hisa yakiropomoka kutokana na kishindo cha mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yaliyoanza siku ya Jumamosi. Pipa moja la mafuta ghafi limefikia karibu dola 80 kwenye soko la dunia ikiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 7.5 ya bei ya wiki iliyopita. …