Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Wanyamapori Duniani, siku maalum inayotambua mchango wa wanyamapori katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Akizungumzia maadhimisho hayo. Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Ephraim Mafuru, amesema kuwa, kwa Tanzania wanyamapori si urithi wa asili pekee bali ni sehemu ya utambulisho wa taifa. “Wanyamapori …