TPA kuwekeza Sh12.1 trilioni kuboresha bandari, kuongeza uwezo wa kupokea shehena

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepanga kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya Sh12.1 trilioni ndani ya miaka 25, ikiwa ni mkakati wa kuongeza uwezo wa bandari kukidhi ongezeko la shehena kutoka tani milioni 32.8 hadi tani milioni 62 ifikapo mwaka 2030/31.