Kesi ya 'Dk Manguruwe’ Shahidi aeleza alivyotapeliwa milioni 1.5 kilimo cha soya

Shahidi wa 20 wa upande wa Jamhuri katika kesi ya kuendesha biashara ya upatu inayomkabili Mkurugenzi wa Vanilla International Ltd, Simon Mkondya, maarufu Dk Manguruwe, ameieleza Mahakama jinsi alivyotapeliwa Sh1.5 milioni kupitia kilimo cha soya.