Kifo cha mwanafunzi, padri awataka waumini wasimlaumu yeyote

Mwili wa mwanafunzi wa darasa la nne, Shule ya Msingi Terrat, Daniel Massawe (11) umeagwa mkoani Arusha huku Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Sinoni Jimbo Kuu la Arusha, Firmini Rudovic akisema hakuna wa kulaumiwa kwa kifo chake.