Kaya 14 zenye jumla ya watu 39 katika Mtaa wa Viwanda, Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro zimekosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa sita usiku wa kuamkia Machi 2, 2026.