Wenyeviti wa vijiji 59 vya Wilaya ya Bahi mwishoni mwa wiki walifanya maandamano hadi ofisi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, wakitaka kusaidiwa kuwasilisha malalamiko yao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).