Kuelekea Siku ya Wanawake Dunia Machi 8,2026, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amesema siyo rahisi kufikia usawa wa kijinsia na mustakabali endelevu wa wanawake bila mchango wa TANESCO. Akiwa mgeni rasmi katika kongamano la wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuhamasisha matumizi ya nishati safi, Gwajima ameahidi kuitangaza TANESCO kwenye Mkutano wa Wanawake utakaofanyika Machi 9,2026 nchini Marekani. “Usawa wa kijinsia na uwezeshaji itakuwa ndoto, mimi kama Waziri mwenye dhamana na wanawake kujidanganya kwamba tutafanikiwa bila mchango wa TANESCO, na umeme wao kufika kwa hawa wanawake na familia zao. Tunafanikiwaje […] The post Gwajima: Si rahisi kufikia usawa wa kijinsia bila mchango wa TANESCO appeared first on SwahiliTimes .