Gwajima awataka wanawake Tanesco kuongoza mapinduzi ya nishati safi ya kupikia

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuendelea kuimarisha kampeni za uhamasishaji wa matumizi ya umeme kwa kupikia, kwa kuweka mkazo katika kubadili mtazamo wa jamii na kuondoa dhana potofu kuhusu gharama za umeme. Waziri Gwajima ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kwenye kongamano …