DMO kahama azomewa, Kihongozi akisikiliza kero za wananchi

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi ametumia takribani saa tatu kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Phantom mjini Kahama, huku Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), Baraka Msumi akizomewa na wananchi wakati akijibu malalamiko ya huduma za afya.