Kituo cha Afya Kataryo kusogeza huduma kwa wananchi

Zaidi ya wakazi 13,200 wa Kata ya Tegeruka pamoja na vijiji jirani katika Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara wanatarajiwa kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya kwa ngazi ya kituo cha afya na kuendelea baada ya Serikali kutoa Sh250 milioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya Kataryo.