Sababu Tanzania kutajwa kuchukua kiti cha uenyekiti wa EAC

Zaidi ya wajumbe 700 kutoka nchi nane wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kuwasili Arusha Jumamosi hii kwa ajili ya mkutano wa 25 wa kawaida wa wakuu wa nchi, unaopangwa kufanyika Machi 7, 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).