Macho na masikio ya wadau wa siasa, sheria na watetezi wa haki za binadamu kesho yataelekezwa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), inayotarajiwa kutoa hukumu katika kesi inayohusu madai ya ukiukwaji wa haki za kiraia na kisiasa wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020 nchini.