MKANDARASI anayejenga Kiwanda cha Uchapaji cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ameongezewa miezi mitatu akamilishe kazi hiyo. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema hayo alipotembelea mradi huo uliopo Makao Makuu ya TSN, Tazara katika Barabara ya Mandela, Dar es Salaam jana. The post Mkandarasi kiwanda cha TSN aongezewa miezi 3 first appeared on HabariLeo .