Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amemwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, kumtafuta popote alipo mkandarasi wa kampuni ya Tunnel Sade Ariana na kumnyang’anya hati yake ya kusafiria kwa kushindwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa bwawa katika mradi wa umwagiliaji wa Ziwa Eyasi.