UONGOZI wa Soko Kuu la Kariakoo umesema takribani asilimia 70 ya wafanyabiashara waliopangiwa vizimba na maduka katika soko jipya tayari wameanza kufanya biashara zao. Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ashraph Abdulkarim, amesema wafanyabiashara wote 1,520 waliokuwa wakifanya biashara katika soko la zamani lililoungua wamepatiwa nafasi katika soko jipya. The post Soko Kariakoo lazidi kunoga first appeared on HabariLeo .