TRA yahimiza kulipa kodi kwa hiari

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewahimiza wananchi kuwa waadilifu na kulipa kodi kwa hiari, ikieleza kuwa ulipaji kodi unaweza pia kuzingatiwa kama sehemu ya ibada. Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, alitoa wito huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na mamlaka hiyo. The post TRA yahimiza kulipa kodi kwa hiari first appeared on HabariLeo .