Operesheni maalumu ilivyonasa meno ya tembo Morogoro

Kamanda Mkama amesema tukio la kwanza lilitokea Machi 14, 2026 katika Kitongoji cha Mambosije Darajani, Kata ya Mlandizi, wilayani Mvomero ambako polisi kwa kushirikiana na askari wa maliasili walimkamata mfugaji mkazi wa Kijiji cha Mangae, Omary Ali (58).