Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa Shilingi bilioni 5.2 kwa Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kuboresha Chuo cha Kikanda cha Mafunzo ya Uhamiaji (TRITA) kilichopo mkoani Kilimanjaro. Amesema juhudi hizo zinalenga kukipanua chuo hicho ili kuanza kutoa elimu katika ngazi ya Shahada, Uzamili na Uzamivu, huku kwa sasa kikitoa mafunzo ya ngazi ya Diploma. Kauli hiyo imetolewa wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Najma Murtaza Giga, kwa lengo la […] The post Rais Samia atoa bilioni 5 kuboresha Chuo cha Uhamiaji cha TRITA appeared first on SwahiliTimes .