Kairuki ataka wadau wa maji kuja na mpango wa kusaidia wenye ulemavu

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amewataka watumishi wa Wizara ya Maji pamoja na wadau wa sekta hiyo kuweka mpango madhubuti wa usawa katika upatikanaji wa huduma za maji kwa watu wenye mahitaji maalumu, wakiwemo wenye ulemavu.