Mkuranga yajadili, kupitisha mpango wa maendeleo ikilenga kuwa na manispaa tatu

Wadau mbalimbali wakiwemo wananchi, taasisi wezeshi na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wamekutana kujadili mpango kabambe wa maendeleo wa wilaya hiyo wa miaka 20 kuanzia mwaka 2026 hadi 2046, wakisisitiza umuhimu wa kuharakisha utekelezaji wake, ili kuendana na kasi ya ukuaji wa eneo hilo.