Waziri Mkuu aagiza walionunua mabati yasiyofaa Katavi wakamatwe

Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba ameagiza kukamatwa kwa watu wote waliohusika na ununuzi wa mabati yasiyokidhi viwango yenye thamani ya takribani Sh200 milioni yaliyokusudiwa kutumika katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Katavi.