Polisi Kilimanjaro yamtia mbaroni mtuhumiwa mauaji ya mfanyabiashara Hai

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Kimira, Kata ya Romu, Wilaya ya Hai, Juma Kimaro (36), kwa tuhuma za kumuua mfanyabiashara Sakina Paulo Tarimo (68).