Wanawake 15 wa kikundi cha Wasikivu katika Mtaa wa Kabangaja, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, wameazisha kiwanda kidogo cha kukaanga na kusaga karanga pamoja na kutengeneza sabuni, baada ya kuwezeshwa mtaji wa Sh11.5 milioni kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Tasaf).