Majaliwa amkumbuka Magufuli kwa uzalendo, ujasiri wa kupambana na maovu

Miaka mitano tangu kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli, kumbukumbu zake zinaendelea kugusa mioyo ya wengi, huku viongozi waliowahi kufanya kazi naye wakikumbuka uongozi wake uliotawaliwa na uchapakazi, uzalendo na msimamo mkali dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.