Wafanyabiashara Mkuti watinga Mahakama Kuu kupinga ujenzi wa soko bila fidia

Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Mkuti lililopo Halmashauri ya Mji wa Masasi, wamefungua shauri la madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara kupinga mpango wa ujenzi wa soko jipya la kisasa katika eneo hilo, bila kufanyika tathmini ya mabanda yao na kulipwa fidia stahiki.