Wanne wauawa kwa tuhuma za uhalifu, kufumaniwa Mbeya

Watu watano wamefariki dunia jijini Mbeya, wakiwamo wanne wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo uporaji na upigaji nondo nyakati za usiku, na mmoja ameuawa kwa fumanizi. Hivi karibuni gazeti la Mwananchi liliripoti uwepo wa makundi ya uhalifu katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya, siku chache baada ya mwandishi wa TV Imaan, Rashid Mkwinda, kuvamiwa, kujeruhiwa na kuporwa.