Mbunge wa Uyole mkoani hapa, Dk Tulia Ackson, amerejesha kicheko kwa waumini 204 wa dini ya Kiislamu, wakiwemo wazee waishio katika mazingira magumu, kwa kutoa futari katika misikiti 17 iliyopo katika kata 13 jimboni kwake.