Polisi watoa tahadhari kuelekea sikukuu ya Eid

Msemaji wa Polisi, David Misime, amesema ulinzi utaimarishwa katika maeneo ya ibada na maeneo ambayo familia, ndugu na marafiki wataona ni sahihi kwenda kusherehekea sikukuu hiyo. Pia, wazazi wameaswa kuwalinda watoto na kutowaacha bila uangalizi, na wananchi kuacha ulinzi majumbani wanaposafiri ili kuzuia wizi na madhara mengine. Mbali na hayo, Jeshi la Polisi limetoa angalizo kwa kila mmoja kuwa na matumizi sahihi ya barabara, kwa kuzingatia kufuata sheria, kanuni na alama zote zilizopo kwenye Barabara ili kuepusha ajali. The post Polisi watoa tahadhari kuelekea sikukuu ya Eid appeared first on SwahiliTimes .