Anwani ‘Nguu za Jadi’ ilivyo faafu kurejelea riwaya

ANWANI ya riwaya hii imeundwa kwa maneno mawili ambayo matumizi yake ni ya kijazanda. Nguu ni vilele vya milima. Neno hili li metumika kijazanda kuashiria upeo wa juu wa mila au tam aduni kandamizi zilipofika hivyo kupuuzwa na kukiukwa na wanaodhulumiwa nazo. Jadi ni mila, desturi na imani za kale ambazo watu wa jamii fulani wameshikilia kwa uzito. Kwa hivyo, Nguu za Jadi ni tam aduni zilizokuwa vikwazo au pingamizi zilizodumaza maen deleo ya jamii. Baadhi ya nguu hi zi za jadi ni kama vile: Mila zinazowadunisha wanawake na kuwanyima uhuru wa kujiendeleza. Kwa mfano Mangwasha pamoja na wanawake wengine hawaruhusi wi kupigania kiti cha kuwa mtemi. Mifumo ya uongozi mbaya chini ya Mtemi Lesulia ilisababisha ufi sadi, ukabila, utabaka, ubinafsi, hali ya kutowajibika, ufujaji wa mali ya umma, uharibifu wa mazingira, uk iukaji wa haki za watoto, ukatili na wizi wa mali ya umma. Umaskini uliokithiri hasa miongoni mwa Waketwa. Ubabedume unaomnyima mwan amke nafasi ya kujieleza kwa mfano Mangwasha angependa kuwaelezea Waketwa wenzake chanzo cha mata tizo yaliyowakumba kuwa ni uhasa ma uliokuwepo tangu jadi baina ya Wakule na Waketwa kuzozania mifugo, chemchemi za maji na mbuga za wan yama lakini inabidi amtafute Lonare ili awaelezee hayo. Mwanamke hak ustahili kumchagua atakayekuwa mumewe. Mangwasha alimkataa Sagi lu ambaye alikuwa tajiri na kuolewa na Mrima ambaye alikuwa maskini li cha ya Chifu Mshabaha kumshurutisha aolewe na rafiki yake. Malezi ya watoto na kukidhi mahita ji ya jamii ni ya mume. Ilikuwa ni lazi ma mwanamke amtegemee mwana mume. Elimu pia ilitengewa wanaume. Mangwasha aligeuka hizi nguu za jadi kwa kupata elimu na kujiendeleza. Aliwalea wana wake na kukidhi ma hitaji yao mumewe alipopotelea kwenye vileo. Vijana wa kike walitumbukizwa katika ukware na matumizi ya mi hadarati na Sihaba. Watu wa kabila dogo na maski ni la Waketwa kama vile Lonare hawakufaa kuchaguliwa kuwa mtemi. Mtoto hawezi kupinga dhu luma za babake, kwa mfano Ngoswe, mwanawe Mtemi Lesulia alivunja nguu za jadi hizi kwa kupinga dhuluma za babake na kumuunga mkono Lonare. Mashauri alimkana ba bake mzazi, Sagilu. Mke hakuruhusiwa kum fuata mumewe kwenye stare he zake. Mangwasha alivun ja nguu hizo na kwenda kumtafuta mumewe Mrima hadi akampata. Mila zinazomnyima mtoto wa kiume nafasi ya kujiende leza. Mila hizi zilimtelekeza mtoto wa kiume kwa kuto thamini elimu na maende leo yake. Tathmini: Jadili tamaduni nyingine kandamizi zilizorejesha maendeleo ya jamii nyuma huku ukirejelea ri waya ya ‘Nguu za Jadi’