Wazawa wajitosa kuendesha taksi mtandao baada ya Uber kuondoka
Ikiwa ni takribani miezi miwili sasa tangu kampuni ya kimataifa ya taksi mtandao ya Uber kufunga shughuli zake nchini, wazawa wameibuka na jukwaa kama hilo wakisema muundo wake umezingatia matakwa na mahitaji ya Watanzania.