NI KATIKA SHULE ZA MSINGI SIMA A NA MADARAKA, IKITIMIZA ILIYOTOLEWA WAKATI WA MSAFARA WA TWENDE BUTIAMA 2025. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na wadau wake wakiwemo Stanbic Bank Tanzania pamoja na waandaaji wa msafara wa Twende Butiama, wamekabidhi rasmi miundombinu ya vyoo katika Shule za Msingi Sima A iliyopo Bariadi mkoani Simiyu pamoja na Shule ya Msingi Madaraka iliyopo Butiama mkoani Mara. Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa wakati wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama uliofanyika Julai mwaka jana, uliolenga kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere huku ukihamasisha maendeleo ya jamii hususan katika sekta […] The post VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAKABIDHI MIUNDOMBINU YA VYOO KWA SHULE MBILI WILAYANI BUTIAMA NA BARIADI appeared first on SwahiliTimes .