Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza Morocco kuwa bingwa wa AFCON 2025, miezi miwili baada ya michuano kumalizika. Senegal amepokonywa ubingwa huo kwa kukiuka kanuni, ambapo Morocco imepewa ushindi wa magoli 3-0 hatua iliyozua mijadala mingi sehemu mbalimbali duniani. Si mara ya kwanza CAF kufanya uamuzi unaozua mjadala. Mnamo Mei 2019, katika mechi ya marudiano ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Espérance de Tunis na Wydad Casablanca, mwamuzi kutoka Gambia, Bakary Gassama, alitangaza Espérance kuwa mabingwa baada ya wachezaji wa Wydad kuondoka uwanjani kufuatia uamuzi wa mwamuzi wa kukataa bao la kipindi cha pili la […] The post Fainali Klabu Bingwa ilivyozua mzozo CAF hadi CAS appeared first on SwahiliTimes .