Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kupitia upya sera na mifumo ya kodi ili kuhakikisha upatikanaji wa taulo za kike (pedi) unakuwa rahisi au bure, hatua itakayosaidia kupunguza changamoto zinazowakabili wasichana hasa walioko vijijini na familia zenye kipato duni.