Ofisa wa benki ahukumiwa kulipa Sh152 milioni kwa wizi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa ofisa wa benki ya Equity Tanzania Limited, Lilian Koka (27), kulipa fidia ya Sh152 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la wizi.