Polisi Dar wakazia marufuku matumizi ya njia za mwendokasi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesisitiza marufuku kwa magari binafsi, ya serikali pamoja na pikipiki kutumia barabara maalum za mabasi yaendayo haraka (BRT), likieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuzuia ajali zinazoweza kusababisha madhara makubwa kwa abiria.