Watatu wafariki ikidaiwa kunywa dawa za kutoa nyongo, kuongeza hamu ya kula

Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Burunga wilayani Serengeti mkoani Mara wamefariki dunia huku mmoja akipelekwa hospitalini baada ya kunywa dawa ya miti shamba waliyopewa kwa lengo la kutoa nyongo tumboni na kuongeza hamu ya kula.