Sheikh Njalambaha awapigia ‘chapuo’ vijana serikalini

Serikali imeombwa kuongeza jitihada za kuwawezesha vijana kiuchumi ili kuwaondoa katika makundi yasiyofaa, huku jamii ikihimizwa kuendeleza matendo mema, mshikamano na kusameheana hata baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.